Vijana 400 wapewa leseni za uchimbaji madini Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza

MWANZA-Serikali imeendeleza jitihada zake za kukuza Sekta ya Madini na kuwasaidia wachimbaj wadogo chini ya uongozi wa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kugawa Leseni ndogo za Uchimbaji Madini (PML) kwa wachimbaji wadogo ili kuwapa fursa ya kuchimba kwenye maeneo yao wenyewe jambo ambalo litapunguza migogoro ya uvamizi wa Leseni na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa jumla.
Zoezi hilo limeongozwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb) leo Julai 18,2026 Wilayani Kwimba mkoani Mwanza, ambapo Jumla ya Leseni 30 za uchimbaji zimegawiwa kwa wachimbaji wadogo wapatao 400 wa Wilaya ya Kwimba na Leseni hizo zinatokana na Leseni kubwa ya utafiti ya ukubwa wa ekari 5,441 iliyofutwa na kurudishwa Serikalini kwa kukosa sifa.
Mheshimiwa Mavunde akielezea matamanio ya Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya kuwasaidia Wachimbaji wadogo amesema hatua inayofuata ni Serikali kupeleka huduma muhimu eneo hilo ili kurahisisha uchimbaji kama vile Ugani, Elimu ya uchimbaji pamoja na Mashine za Kuchoronga zilizonunuliwa na Serikali kwajili ya wachimbaji wadogo.

“Hizi ndio zile leseni ambazo zinafutwa kwa kushindwa kukidhi masharti ya utoaji wake ambapo kwa sasa tutazipanga vyema kwa uwekezaji mkubwa na kwa wachimbaji wadogo.

"Kwa sasa tutahakikisha kupitia programu ya 𝙈𝙞𝙣𝙞𝙣𝙜 𝙛𝙤𝙧 𝙖 𝘽𝙧𝙞𝙜𝙝𝙩𝙚𝙧 𝙏𝙤𝙢𝙤𝙧𝙧𝙤𝙬(𝙈𝘽𝙏) kundi kubwa la vijana na wakina mama wanapata Leseni na kufanya uchimbaji pasipo changamoto yoyote.
"Kwa sasa wananchi waache kuvamia Leseni za watu kwa kuwa hivi sasa Serikali inaendelea na zoezi la kufuta leseni nchi nzima zinazomilikiwa kiholela na kuwapa wachimbaji wadogo ili wachimbe kwenye maeneo yao wenyewe huku wakiwa upande salama kisheria,”amesema Mavunde.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Ng’wilabuzu Ludigija ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia sera zake za kuwasaidia wachimbaji wadogo na kuwataka wachimbaji wadogo kuzitumia vyema Leseni husika kwa maendeleo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here