Waziri wa Fedha awasili mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku tatu

TANGA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewasili mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku tatu yenye lengo la kutembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi miradi ya maendeleo, kuimarisha utoaji wa huduma za kifedha na forodha, pamoja na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara.
Mhe. Balozi Omar amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mheshimiwa Dadi Kolimba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dkt. Batida Buriani na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, Naibu kamishna wa Huduma za kiufundi, Bw. Ted Silkiluwasha, Meneja TRA TANGA, Bw. Castro John, viongozi na maafisa wengine waandamizi wa Serikali.

Katika ziara hiyo, Mhe. Balozi Omar atatembelea Bandari ya Tanga na Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Horohoro, ambako atapata taarifa kuhusu utendaji wa huduma na hatua zinazochukuliwa kuboresha biashara na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Aidha, atakagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na kuweka jiwe la msingi katika baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo, ambapo pia atakutana na watumishi wa Ofisi za Hazina Ndogo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga, kwa lengo la kujadili masuala ya utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katika kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi, Mhe. Balozi Omar, atafanya kikao na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga, ambapo atasikiliza maoni yao na kujadiliana kuhusu fursa na changamoto zinazohusu biashara, uwekezaji na mazingira ya uchumi.
Sambamba na shughuli hizo, Mhe. Balozi Omar atashiriki hafla ya ugawaji wa miguu bandia kwa wananchi wenye mahitaji maalumu na kushuhudia utoaji wa mafunzo kwa makundi maalumu kuhusu namna ya kushiriki zabuni za Serikali kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuongeza ushiriki wa makundi hayo katika fursa za kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here