Babu jela maisha kwa kumbaka kitukuu wake

DAR-Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha jela, Amoni Amandusi Mtwanga miaka 72 mkazi wa Pugu kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 10. Hukumu hiyo ilitolewa katika Kesi namba CC 3920/2026 iliyosikilizwa mbele ya Hakimu Mohamed Burhani.
Kwa mujibu wa mashtaka, tukio hilo lilitokea tarehe 16/11/2025. Mhanga ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la III Shule ya Msingi Kigogo, makazi Pugu Kigogo, alidaiwa kufanya ngono na mtuhumiwa njiani alipokuwa akitoka shuleni. Njia ya mtoto ilikuwa karibu na geti la nyumba ya mtuhumiwa ambaye anaishi peke yake bila familia.

Mahakama iliambiwa kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alimwita mtoto huyo, akamuingiza ndani hadi chumbani na kumfanyia kitendo hicho kwa kumlazimisha kuvua nguo huku akimziba mdomo ili asipige kelele. Pia ilidaiwa kuwa mzee huyo alikuwa amemfanyia kitendo hicho zaidi ya mara moja na baada ya kila tukio alikuwa akimpa mtoto shilingi 1000 ili asimweleze mzazi wake.

Uhalifu huo ulibainika baada ya mama wa mtoto, Aisha Salum, kugundua mabadiliko kwa binti yake na kumuuliza. Mtoto ndipo alimtaja mzee huyo kuwa ndiye anayemfanyia kitendo hicho. Mama alitoa taarifa na kesi ikafunguliwa mahakamani.

Baada ya kusikiliza ushahidi wote, Hakimu Mohamed Burhani alimkuta mtuhumiwa na hatia na kumhukumu kifungo cha maisha jela. Mahakama imesema hukumu hiyo ni fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here