Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaendelea kutoa elimu ya uchumi na fedha Maonesho ya Nane Nane

DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania inashiriki katika Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) ambayo yanafanyika kitaifa viwanja vya Nane Nane Nzuguni mkoani Dodoma.
Benki Kuu pia inashiriki katika Maonesho hayo katika Viwanja vya Dole Kizimbani Unguja Zanzibar, Viwanja vya John Mwakangale Mbeya, Viwanja vya Nane Nane Nyamhogolo Mwanza, Viwanja vya Ngongo Lindi na Viwanja vya Nane Nane Njiro Arusha.

Miongoni mwa viongozi waliotembelea Banda la BoT Mbeya ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa, ambaye ameipongeza Benki Kuu kwa kuendelea kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi na kifedha yanayowezesha wananchi mkoani humo kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Kupitia Maonesho haya, BoT inatoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ikiwemo kuandaa na kusimamia sera ya fedha ambayo inalenga kudhibiti mfumuko wa bei ambao ni msingi wa ukuaji endelevu wa uchumi, pamoja na uwekezaji katika dhamana za serikali za muda mfupi na mrefu.

Benki Kuu Pia, inatoa elimu ya namna inavyosimamia mabenki na taasisi za fedha ili ziwe imara na ziweze kutoa mikopo kwa sekta za uzalishaji, kuendeleza jumuishi wa kifedha kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za benki na malipo ya kidijitali yanayorahisisha biashara.
Vilevile, wananchi wanaelezwa kuhusu kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa huduma za kifedha, masuala ya ajira na utumishi ndani ya Benki Kuu, pamoja na utambuzi wa alama za usalama zilizopo kwenye noti za Tanzania na namna ya kuzitunza.

Maonesho hayo, yenye kaulimbiu “Tambua Soko, Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050,” yanafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here