DAR-Naibu Gavana wa BoT anayesimamia Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi Mpya wa Shirika la Fedha la kimataifa (IMF) Bi. Jana Bricco, katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam aliyefika kujitambulisha baada ya kuanza kazi rasmi mwezi Agosti 2026.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo Agosti 21, 2026, Dkt. Yamungu Kayandabila amemuhakikishia kuwa, Benki Kuu itaendeleza ushirikiano na taasisi hiyo katika ufadhili na utekelezaji wa miradi ya kimkakati pamoja na programu mbalimbali za kusimamia na kustawisha sekta ya fedha na uchumi wa nchi kiujumla.
Kwa upande wake, Bi. Jana Bricco, ambaye amechukua nafasi ya Mwakilishi Mkazi aliyemaliza muda wake, Bw. Sebastian Acevedo, ameahidi kuendeleza ushirikiano kati ya IMF na Tanzania katika masuala mbalimbali ya ustawi wa uchumi ikiwemo kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Gavana anayesimamia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Msemo, Naibu Gavana anayesimamia Utawala na Udhibiti wa Ndani, Dkt. Rahma Mahfoudh pamoja na viongozi wengine wa Benki Kuu.
Tags
Benki Kuu ya Tanzania
Dira 2050
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Habari
International Monetary Fund (IMF)
Kimataifa











