DAR-Kamanda wa Kikosi cha Polisi TAZARA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP Johari S.Said amefanya ziara ya ukaguzi wa kituo cha Polisi Tazara Pugu Wilaya ya Temeke Road mkoani Dar es Salaam kwa lengo la kufatilia utendaji kazi pamoja na kuhakikisha jamii inapata huduma bora.
SACP Johari amefanya ziara hiyo ya ukaguzi leo Agosti 21,2026 pamoja na kufuatilia kwa karibu utayari wa askari.SACP Johari amewataka askari hao kuwa weledi katika kutoa huduma bora kwa jamii. "Nidhamu na weledi katika majukumu yetu inahitajika sana,jamii imejenga imani kubwa juu yetu,hivyo ni lazima tuwajibike kwa kuwa wanachokihitaji kutoka Jeshi la Polisi,"amesema.


