Jela maisha kwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 11 jijini Tanga

TANGA-Mahakama ya Mkoa wa Tanga imemhukumu Said Yunusu maarufu kama Big Sela, mwenye umri wa miaka 20 na mkazi wa Makorora jijini Tanga, kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 11.
Akisoma hukumu hiyo tarehe 24 Agosti 2026, Hakimu Mhe. Mwanaheri amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka na hivyo kujiridhisha kuwa kosa hilo limethibitishwa dhidi ya mshtakiwa.

Hakimu huyo amesema hukumu hiyo imetolewa kwa kuzingatia sheria na kuhakikisha haki inatendeka, huku ikiwa ni fundisho kwa watu wengine wanaoweza kujihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Kwa mujibu wa maelezo ya kesi, mtuhumiwa alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumlawiti mtoto huyo mwenye umri wa miaka 11, ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la Nne.

Kesi hiyo yenye Namba CC No. 2829/2026 ilisikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Tanga, ambapo baada ya kusikiliza ushahidi uliowasilishwa, Mahakama ilimkuta Said Yunusu maarufu kama Big Sela na hatia.

Mahakama imemhukumu mtuhumiwa huyo kutumikia kifungo cha maisha jela.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here