TANGA-Rahimu Gumbo, mwenye umri wa miaka 43 na mkazi wa Chongoleani jijini Tanga, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Mkoa wa Tanga baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12.
Hukumu hiyo imetolewa tarehe 24 Agosti 2026 na Hakimu Mhe. Mwanaheri, baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi uliowasilishwa katika kesi hiyo na kujiridhisha kuwa shtaka dhidi ya mshtakiwa limethibitishwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya kesi, manusura wa tukio hilo ni mwanafunzi wa Darasa la Sita mwenye umri wa miaka 12, ambaye alifanyiwa kitendo hicho kinyume na sheria.
Kesi hiyo yenye Namba CC No. 7726/2026 imehitimishwa kwa Mahakama kumtia hatiani Rahimu Gumbo na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela, kwa mujibu wa sheria.
Hukumu hiyo ni sehemu ya hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia, hususan dhidi ya watoto.
