Jela miaka 30 kwa tuhuma za ubakaji

MOROGORO-Mahakama ya Wilaya ya Kilombero imemhukumu Isaya Joel Ndemo kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji katika shauri la jinai namba MLB/IR/788/2025, lililohusisha tukio lililotokea tarehe 21 Novemba 2025 majira ya saa 06:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa za shauri hilo, mtuhumiwa alidaiwa kumvizia mlalamikaji akiwa shambani, kisha kumkaba shingoni na kumfanyia kitendo cha ubakaji.

Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Kilombero tarehe 05 Januari 2026 ambapo shauri hilo liliendelea kusikilizwa na upande wa mashtaka kuwasilisha ushahidi. Baada ya kusikiliza na kupitia ushahidi uliowasilishwa, mahakama ilimtia hatiani kwa kosa hilo na kutoa hukumu tarehe 19 Agosti 2026.

Katika hukumu hiyo, Mahakama ya Wilaya ya Kilombero imemwamuru Isaya Joel Ndemo kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani pamoja na kulipa fidia ya shilingi 500,000 kwa mlalamikaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here