Siku tano za kusherehekea utamaduni wa Tanzania mkoani Morogoro

MOROGORO-Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amesema kuwa, Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika kila mwaka lina lenga kufungamanisha Uchumi, Utalii na Urithi wa Tanzania pamoja na kuusherehekea.
Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 23, 2026 katika ya Kambi ya Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini iliyopo eneo la Mazimbu, Mkoani Morogoro, kuhusu Tamasha la 4 la Kitaifa la Utamaduni linaloanza tarehe 25 hadi 29 katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani hapo.

Amesema, Tamasha hilo litakua na matukio mbalimbali ikiwemo mdahalo wa maadili na kuwaomba watanzania kujitokeza kujadili namna ya kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili. 

Akiongeza kuwa kurakua na Mbio (Jogging), Michezo ya asili kama vile karata, bao na drafti, mashindano ya ngoma, muziki na maonesho ya vyakula.

"Watanzania tulinde tamaduni ikiwemo mavazi, ngoma na vyakula vyetu vya asili pia tuendelee kujenga Utanzania wenye Umoja na mshikamano," amesema Msigwa.

Ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Watanzania wa mkoa wa Morogoro na mikoa jirani kushiriki Tamasha hilo ili kusherehekea Utamaduni na kuweza kuurithisha kizazi cha sasa na baadae.

Akiongeza kuwa washiriki tayari wameanza kuingia mkoani hapo kusherehekea mila na deaturi za kitanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here