Kamanda Chilya awauma sikio askari mpakani mwa Tanzania na Msumbiji

RUVUMA-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),Marco G. Chilya amefanya ziara ya kutembelea na kukagua askari katika maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Katika ziara hiyo, SACP Chilya amekagua utendaji wa askari, hali ya ulinzi katika maeneo ya mpakani pamoja na namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Kamanda Chilya SACP amewataka askari hao kuendelea kuwa makini, waadilifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi wakati wote wanapotekeleza majukumu yao huku akisisitiza umuhimu wa kulinda mipaka ya nchi, kuzuia uhalifu wa aina mbalimbali na kuhakikisha usalama wa wananchi wanaoishi katika maeneo ya mpakani.
Kwa upande wao, askari wanaotekeleza Operesheni Kambale wamemueleza Kamanda Chilya kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa umakini, weledi na ushirikiano, huku wakihakikisha maeneo ya mpakani yanaendelea kuwa salama kwa wananchi na shughuli zao za kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here