Magazeti leo Agosti 23,2026

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema CCM inalenga kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia saba ifikapo mwaka 2030, huku ukichochea ongezeko la kipato na kuboresha maisha ya wananchi.
Wasira amesema hayo Agosti 21,2026 wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM mkoani Singida, akieleza kuwa ukuaji wa uchumi hautakuwa na maana iwapo hautaonekana katika maisha ya mtu mmoja mmoja kupitia ongezeko la kipato na fursa za kiuchumi.

Amesema katika Ilani ya CCM, chama hicho kimeweka msisitizo wa kukuza uchumi jumuishi unaolenga kumwezesha kila Mtanzania kunufaika na ukuaji wa uchumi.




Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here