DODOMA-Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wameendelea kutoa huduma ya msaada wa kisheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea kwenye viwanja vya John Samweli Malecela vilivyopo jijini Dodoma.
Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakielimisha wananchi majukumu ya Ofisi hiyo walipotembelea banda la maonesho la Ofisi hiyo wakati wa maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Samweli Malecela jijini Dodoma.
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Salehe Manoro akitoa elimu ya msaada wa kisheria bila malipo kwa Bi.Iptisam Salum alipotembelea banda la maonesho la Ofisi hiyo wakati wa maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Samweli Malecela Jijini Dodoma.
Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakielimisha wananchi majukumu ya Ofisi hiyo walipotembelea banda la maonesho la Ofisi hiyo wakati wa maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Samweli Malecela jijini Dodoma.
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Salehe Manoro akitoa elimu ya msaada wa kisheria bila malipo kwa ndugu Mosses Ibrahim alipotembelea banda la maonesho la Ofisi hiyo wakati wa maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Samweli Malecela Jijini Dodoma.Kupitia Maonesho ya Nanenane, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na kuitangaza Ofisi na kuendelea kujenga Mahusiano kati ya ofisi hiyo,wadau na wananchi.
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inawakaribisha wananchi na wadau wa Mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani kuendelea kutembelea banda la Ofisi hiyo ili waweze kupata huduma zinazotolewa ndani ya banda hilo.



