Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu (Mb) Agosti 8, 2026 amefanya vikao kazi jijini Dar es salaam na Menejimenti za taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji.







Katika vikao kazi hivyo, Waziri Sangu, kwa nyakati tofauti amekutana na Menejimenti za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Mashirika ya Umma (PSSSF); Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF); Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF); na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).Waziri Sangu amepokea taarifa za utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo kutoka kwa watendaji wake wakuu na kuelekeza taasisi hizo kuendelea kuongeza ufanisi hususan katika matumizi ya teknolojia ya Habari na mawasiliano (TEHAMA) katika utendaji na utoaji huduma kwa wananchi.
“Nawaelekeza kuongeza utoaji wa elimu ya matumizi ya kidijitali katika mifumo yetu ili kuwawezesha wale wasio na elimu ya kidijitali kupata huduma zetu kwa urahisi na haraka,” amesema Waziri Sangu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














