DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza Johari, Agosti 4, 2026 jijini Dar es Salaam amekutana na Menejimenti ya Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (TIArb) kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.
Menejimenti hiyo imetoa shukrani kwa Mhe. Johari kwa ushiriki wake katika Mkutano wa Nane wa Mwaka wa TIArb na Wiki ya Usuluhishi ya Dar es Salaam (DAR Arbitration Week), uliofanyika Julai 22, 2026, jijini Dar es Salaam.
Vilevile imemuahidi Mhe. Hamza Johari kutekeleza ushauri aliowapa wakati wa mkutano huo ikiwemo kuweka mpango wa utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo, uliojumuisha wadau wa usuluhishi na uwekezaji ndani na nje ya nchi.
Aidha, Rais wa TIArb, Wakili Aderickson Njunwa, amemkabidhi Mhe. Johari zawadi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kuendeleza usuluhishi nchini.
Miongoni mwa walioshiriki katika kikao hicho kutoka TIArb ni Katibu wa Heshima, Wakili Marydensia Katemana; Mweka Hazina, Wakili Sultan Rajab; Mjumbe wa Baraza, Wakili Theofil Kimaro; Mjumbe wa Baraza, Wakili Nasra Songoro; Katibu Mtendaji, Maria Mruma; na Afisa wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (TEHAMA), Mhandisi Silvanus Agapt.



