Mwanasheria Mkuu wa Serikali,CMT wajadili ufanisi wa sheria za masoko ya mtaji

DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari,Agosti 4,2026 jijini Dar es Salaam, amekutana na Msajili wa Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT), Dkt.Martin Wilbert Kolikoli, kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji wa Baraza hilo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Johari amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea kupitia sheria mbalimbali za nchi kuwezesha utekelezaji wa Dira 2050 na kuongeza ufanisi katika utendaji na utoaji wa huduma.

Vilevile Mhe. Johari amesisitiza kwamba Masoko ya mtaji ni nyezo muhimu katika utekelezaji wa Dira 2050, hivyo ni muhimu sheria zake zikaendana na dira hiyo na kasi ya maendeleo ulimwenguni.
Kwa upande wake, Dkt. Kolikoli ameeleza majukumu ya Baraza la Masoko ya Mitaji pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake.

Pia amependekeza maboresho ya sheria zinazohusu masoko ya mitaji, dhamana na soko la bidhaa, hususan katika maeneo ya ulinzi wa haki na utatuzi wa migogoro.
Dkt. Kolikoli amemkabidhi Mhe. Johari jarida la CMT pamoja na kutoa wito kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kushirikiana na CMT katika kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya masoko ya mtaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here