Polisi Mbeya mabingwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini

RUKWA-Timu ya mpira wa miguu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya imeibuka bingwa wa mashindano ya mpira wa miguu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kuwafunga goli moja kwa bila Polisi Mkoa wa Songwe.
Akizungumza mara baada ya fainali hiyo iliyochezwa Agosti 10, 2026 mkoani Rukwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema kuwa, ushindi huo umetokana na maandalizi mazuri ya timu, umoja na mshikamano.

Aidha, Kamanda Kuzaga amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi na vikundi vya hamasa kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake hadi kupata matokeo mazuri na kusisitiza nidhamu kuelekea maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi Jamii ambapo timu hiyo itashindana na timu kutoka kanda nyingine.

Mashindano hayo ya kikanda yalifunguliwa rasmi Agosti 09, 2026 yalishirikisha timu za mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha, kuvuta kamba na michezo mingine ya jadi ikijumuisha mikoa ya Rukwa (Mwenyeji), Mbeya, Songwe na Katavi ikiwa ni maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi Jamii yatakayofanyika Agosti 25, 2026 mkoani Mbeya.

Aidha,maadhimisho hayo yanabeba kauli mbiu inayosema, Miaka 20 ya Polisi Jamii: Tushirikiane kuimarisha Amani, Usalama na Umoja wa Kitaifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here