PSSSF yawajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii

DAR-Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza uelewa wa umma na wanachama kuhusu huduma, haki na wajibu unaotolewa na Mfuko huo.
Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda ya Kinondoni, Bw. Costa Mpagike (aliyesimama), kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari kuhusu Hifadhi ya Jamii ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza uelewa wa umma na wanachama kuhusu huduma, haki na wajibu unaotolewa na Mfuko huo. Ufunguzi wa mafunzo hayo ulifanyika Agosti 17, 2026. Wengine pichani ni Afisa Uhusiano Mkuu PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto) na Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Nevile Meena.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Agosti 17, 2026, yalifunguliwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Kinondoni, Bw. Costa Mpagike, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo.
Afisa wa Mfuko wa PSSSF, Bi. Harrieth Shoo, akiwasilisha mada kuhusu Haki na wajibu wa wanachama na waajiri pamoja na ushughulikiaji wa ucheleweshaji wa michango na mafao wakati wa semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na PSSSF na kufanyika kwenye jengo la PSSSF commercial complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Bw. Mpagike alisema lengo kuu ni kujenga na kuimarisha uhusiano wa kudumu kati ya PSSSF na vyombo vya habari ili kuwezesha utoaji wa taarifa sahihi kwa umma kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii.

“Kama mjuavyo, mafunzo haya ya siku mbili yanalenga kujenga na kuimarisha uhusiano wa kudumu na vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari, kuongeza uelewa wa umma na wanachama kuhusu shughuli za PSSSF, haki na wajibu wao kupitia mada mbalimbali za mafunzo, uzalishaji wa makala za uchambuzi na kupunguza upotoshaji wa taarifa,” alisema Bw. Mpagike.
Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa PSSSF, Bw. Adoulph Mhechella, akitoa mada kuhusu Sera na mkakati wa uwekezaji wa PSSSF (miradi ya kimkakati na ulinzi wa fedha za wanachama) kwenye mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari.

Afisa wa PSSSF, Bw.Ramadhan Sossora, akiwasilisha mada kuhusu Hifadhi yaJamii na ijue PSSSF, wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika kwenye jengo la PSSSF commercial complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam kuanzia Agosti 17-18, 2026.
Afisa wa PSSSF, Bw.Mohammed Nyallo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao mbalimbali yanayotolewa na PSSSF na jinsi ya kuyaomba, wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika kwenye jengo la PSSSF commercial complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam kuanzia Agosti 17-18, 2026.

Aliongeza kuwa,mbali na kuwapatia maarifa kuhusu mifumo na huduma za PSSSF, Mfuko unatamani washiriki wa mafunzo hayo wawe mabalozi wa kueneza taarifa sahihi za hifadhi ya jamii katika vyumba vya habari na kwenye jamii kwa ujumla.

“Tutawajengea uwezo ili muwe na taarifa sahihi kuhusu PSSSF na huduma zake, jambo ambalo litawarahisishia kuandika habari kwa ukweli, weledi na usahihi zaidi,”alisisitiza.
Afisa wa PSSSF, Bw.Mohammed Nyallo, akiwasilisha mada kuhusu Mafao mbalimbali yanayotolewa na PSSSF na jinsi ya kuyaomba, wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mfuko huo na kufanyika kwenye jengo la PSSSF commercial complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam kuanzia Agosti 17-18, 2026.

Baadhi ya washiriki walieleza kufurahishwa na fursa hiyo ya mafunzo, wakisema elimu waliyoipata itawasaidia kuboresha kazi zao za uandishi wa habari, hususan katika kuripoti masuala ya hifadhi ya jamii.

Mratibu wa mafunzo hayo, Bw. Nevile Meena, amesema elimu waliyoipata iwasaidie katika shughuli zao za uandishi wa habari.
Waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo maalum ya siku mbili kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii, iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ikiwa ni jitihada za kuongeza uelewa wa umma na wanachama kuhusu huduma, haki na wajibu unaotolewa na Mfuko huo. Mafunzo hayo yaliyoanza Agosti 17, 2026 yamekamilika Agosti 18, 2026 kwenye Jengo la PSSSF commercial complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam.
“Kama hujui kitu huwezi kuandika kwa usahihi, kama unafahamu jambo utaandika kwa usahihi, nawashukuru PSSSF kwa kutujengea uelewa, mimi binafsi nimekuwa mwandihi wa habari wa siku nyingi lakini kuna vitu vingine nimevifahamu sasa kujifunza hakuna mwisho. Naamini tutayatendea haki haya mafunzo na tutafanya vizuri katika kazi zetu,”amesisitiza Bw. Meena.

Mwandishi wa habari kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Bi. Zena Chande, alisema mafunzo hayo yamemsaidia kuongeza uelewa kuhusu huduma na mafao yanayotolewa na PSSSF.

“Kimsingi nimeongeza uelewa kuhusu namna PSSSF inavyotekeleza majukumu yake. Mambo tuliyojifunza hapa yatanisaidia kufanya kazi yangu kwa ubora zaidi. Kabla ya mafunzo haya sikuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kiinua mgongo, pensheni na sifa za kufaidika na mafao hayo, lakini sasa nimeelewa kwa kiwango kikubwa,” amesema Bi. Chande.
Waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo maalum ya siku mbili kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii, iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ikiwa ni jitihada za kuongeza uelewa wa umma na wanachama kuhusu huduma, haki na wajibu unaotolewa na Mfuko huo. Mafunzo hayo yaliyoanza Agosti 17, 2026 yamekamilika Agosti 18, 2026 kwenye Jengo la PSSSF commercial complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam.
“Ni mafunzo yenye tija kubwa sana kwetu sisi waandishi wa habari ambao tuna nafasi kubwa ya kuwasiliana na jamii wakiwemo wanachama wa PSSSF,” amesema Bi. Julieth Robert, mwandishi wa habari wa ITV.

Kwa upande wake, mwandishi wa habari mkongwe ambaye kwa sasa ni mnufaika wa pensheni kutoka PSSSF, Bw. Beda Msimbe, alitoa ushuhuda kuhusu umuhimu wa pensheni katika maisha ya mstaafu.

“Hii pensheni inanisaidia sana katika maisha yangu ya kila siku. Baada ya kustaafu, changamoto za maisha zipo, lakini mimi ninafurahia kuwa mwanachama wa PSSSF. Sasa ni mstaafu ninayepokea pensheni kila mwezi. Kila inapofika tarehe 22 napokea ujumbe mfupi wa simu unaonijulisha kuwa fedha zimeingizwa kwenye akaunti yangu. Kwa kweli, PSSSF wanatekeleza jukumu lao vizuri,”amesema Bw. Msimbe.
Waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo maalum ya siku mbili kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii, iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ikiwa ni jitihada za kuongeza uelewa wa umma na wanachama kuhusu huduma, haki na wajibu unaotolewa na Mfuko huo. Mafunzo hayo yaliyoanza Agosti 17, 2026 yamekamilika Agosti 18, 2026 kwenye Jengo la PSSSF commercial complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es salaam.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa PSSSF wa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali hususan vyombo vya habari katika kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii na huduma zinazotolewa na mfuko huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here