DODOMA-Kiasi hicho kimewasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira katika kikao chake bungeni jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) akiongoza kamati hiyo pamoja na taratibu zitakazochukuliwa, kamati imeshauri na kuelekeza madai kufanyiwa kazi ili Serikali iendelee kuimarisha huduma ya maji kwa wananchi.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema moja ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuanza kutumika kwa matumizi ya Dira janja za malipo kabla ambapo deni hukusanywa kila malipo ya huduma ya maji yanapofanyika na kufanya mazungumzo na wadaiwa ili kuona namna bora ya kupunguza madai hayo.
Waziri Aweso ameainisha kuwa ili huduma ya maji imfikie mteja, nyuma yake zipo gharama kadhaa za uendeshaji ikiwemo nishati ya umeme, dawa za kutibu maji, rasilimaliwatu, na matengenezo.
Amesema mteja anapowajibika kulipa bili ni moja ya mchango wake katika kuimarisha na kuendeleza huduma ya maji nchini.








