FARIDA RAMADHANI
NA SAIDINA MSANGI
SERIKALI imewaagiza wataalamu wanaosimamia mipango na bajeti katika wizara na taasisi mbalimbali nchini kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma ili kuboresha utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,Bw. Nsubili Joshua kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt.Natu El-Maamry Mwamba wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea,wakala za Serikali.
Sambamba na Sekretarieti za mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square jijini Dodoma.
Amesema,ni muhimu kwa wataalamu hao kuwa na vikao vya kamati za bajeti kwa ajili ya kupanga, kuweka vipaumbele na kugawana rasilimali fedha za mafungu yao, akisisitiza utekelezaji wa majukumu ya taasisi kwa mujibu wa bajeti iliyoidhinishwa.
‘‘Nasisitiza muandae na kuhuisha mipango mikakati ya taasisi zenu kwa kuwianisha na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka 5 (FYDP IV), na mipango mingine ya sekta,"amesema Bw. Joshua.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, akizungumza wakati akifungua
kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Ameongeza kuwa,ni muhimu kwa wataalamu hao kuandaa mipango na bajeti za mafungu yao kwa kuzingatia mipango ya kisekta ili kufaidika na ushirikiano wa pamoja.
Pia, amewahimiza wataalamu hao kushiriki kikamilifu na kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha na kuongeza ufanisi katika utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali pamoja na kuboresha Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali wa mwaka 2027/28-2029/30.
Bw. Joshua amesema,ushiriki wao katika kikao hicho unaashiria kujitolea kwa pamoja katika kuboresha utekelezaji na usimamizi wa bajeti ya Serikali, kuongeza ufanisi katika mchakato wa bajeti na kuhakikisha vipaumbele vya Serikali vinatekelezwa ipasavyo.
Kaimu Kamishna wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Raymond Kwohelera, akitoa maelezo ya awali katika kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Amebainisha kuwa,kikao hicho kilikuwa jukwaa muhimu la kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/26 na Maandalizi ya Bajeti ya Serikali wa mwaka 2026/27.
Ni ili kubaini maeneo yanayohitaji maboresho kwa lengo la kupata maoni na kuweka mikakati itakayotusaidia kuboresha uandaaji wa mipango na bajeti kwa mwaka 2027/28-2029/30.
Aidha, amewafahamisha kuwa mchakato wa maandalizi ya Mwongozo wa Mpango na Bajeti ya mwaka 2027/28-2029/30 umeanza na kubainisha kuwa Mwongozo huo ni nyenzo muhimu katika maandalizi ya Mipango na Bajeti za mafungu yao.
Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Serikali, Bw. Juma Mfaume akitoa mada katika kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
“Ushauri na mapendekezo yatakayotokana na kikao hiki yatasaidia katika kuboresha maandalizi ya Mwongozo huu.Nichukue fursa hii kuwaasa washiriki wote, kutumia fursa hii vizuri ili tuweze kupata Mwongozo wa maandalizi ya bajeti na bajeti ya Serikali nzuri na inayotekeleza kwa mwaka 2027/28-2029/30,"amesema Bw.Joshua.
Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Raymond Kwohelera ameeleza kuwa,kikao hicho hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kutoa fursa kwa wataalamu na wadau kujadili kwa kina changamoto zinazojitokeza katika mchakato wa bajeti, pamoja na kutoa mapendekezo ya namna ya kuzitatua.
Meza kuu ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, Kaimu Kamshina wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Raymond Kwohelera na Kamishna Msaidizi wa Idara hiyo, Bw. Fundi Makama, wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya maandalizo ya kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.
Meza kuu ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Nsubili Joshua, Kaimu Kamshina wa Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Raymond Kwohelera na Kamishna Msaidizi wa Idara hiyo, Bw. Fundi Makama, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikia wa kikao kazi cha Tathmini ya Uandaaji na Utekelezaji wa Bajeti kwa watalaam kutoka wizara, idara zinazojitegemea, wakala za Serikali na sekretarieti za mikoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kinachofanyika katika ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).
Amebainisha kuwa,katika hatua hiyo wamehusishwa wataalamu kutoka wizara, sekta na taasisi mbalimbali, ambao wanatarajiwa kushirikiana katika kupitia utekelezaji wa bajeti, kubaini maeneo yenye changamoto na kuweka mikakati ya kuboresha mchakato huo.





