Usikimbilie ahadi za faida kubwa-BoT

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wananchi wote kutambua kuwa, ahadi za faida kubwa na za haraka zinaweza kuonekana kuvutia, lakini zinaweza pia kuambatana na hatari kubwa ya kupoteza fedha zao.
Kwa mujibu wa BoT, kabla ya kuwekeza, chunguza kwa makini mpango unaoelekezwa na hakikisha unaelewa unavyofanya kazi, chanzo cha faida kinapotoka na hatari zinazoweza kujitokeza.

"Usikubali kutoa fedha katika mpango ambao hauuelewi au ambao unaahidi faida kubwa bila maelezo ya kutosha.Aidha, thibitisha uhalali wa taasisi au mtoa huduma wa fedha kabla ya kutoa fedha zako.

"Usifanye uamuzi kwa sababu umeambiwa na rafiki, ndugu au kwa sababu umeona watu wengi wakijiunga. Tafuta taarifa sahihi kutoka vyanzo rasmi na hakikisha mtoa huduma ameidhinishwa na mamlaka husika."

Pia, BoT imesisitiza kuwa,usikubali presha au tamaa ya kupata faida ya haraka ikufanye utoe fedha zako bila kufanya uchunguzi wa kutosha.

Faida kubwa ya haraka? Usikimbie-chunguza kwanza!

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here