Viongozi wa wanafunzi kutoka vyuo 12 vya elimu ya juu mkoani Dar es Salaam wafanya ziara SGR

DAR-Viongozi wa wanafunzi kutoka vyuo 12 vya elimu ya juu mkoani Dar es Salaam, wakiwemo Marais, Mawaziri Wakuu, Makamu wa Rais na Maspika wa Bunge wa serikali za wanafunzi, wametembelea Mradi wa Reli ya Standard Gauge (SGR) katika Jengo la Stesheni ya John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo imelenga kuwapa viongozi hao fursa ya kujifunza na kupata uelewa kuhusu maendeleo, uendeshaji na mchango wa SGR katika kuboresha usafiri na usafirishaji nchini.

Vyuo vilivyoshiriki ziara hiyo ni pamoja na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Dar es Salaam Maritime Institute (DMI), Tanzania Institute of Accountancy (TIA), DARTU, Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chuo cha Takwimu, Institute of Finance Management (IFM), College of Business Education (CBE) na DUCE.

Ziara hii imeanzia SGR kipande cha kwanza inaendelea kwa vipande vyote vya ujenzi wa SGR ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa kwa vijana kuhusu miradi ya kimkakati ya taifa na nafasi ya sekta ya reli katika kukuza uchumi na maendeleo ya Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here