Waziri Kombo amuaga Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana na kuagana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Christine Grau, kufuatia kukamilika kwa muda wake wa uwakilishi nchini.
Katika mazungumzo yao, Mheshimiwa Waziri Kombo alimpongeza Balozi Grau kwa mchango wake katika kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, hususan katika maeneo ya ushirikiano wa maendeleo, biashara na uwekezaji, Global Gateway, sekta binafsi, pamoja na majadiliano ya wazi kati ya pande hizo mbili.
Ameelezea azma ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika misingi ya kuheshimiana, uwazi na manufaa ya pande zote, huku akimtakia Balozi Grau kila la kheri katika majukumu yake yajayo.
Kwa upande wake, Balozi Grau aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata katika kipindi cha uwakilishi wake nchini, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kimkakati kupitia majadiliano ya wazi na ushirikiano wa katika sekta muhimu maendeleo, kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here