Waziri Kombo apokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Sweden nchini Tanzania

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Ingrid Johansson, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Baada ya tukio hilo viongozi hao wamejadili namna bora ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden, hususan katika maeneo ya biashara na uwekezaji.

Akizungumza na Balozi huyo, Mhe. Waziri Kombo ameeleza kuwa umuhimu wa ongezeko la biashara kati ya Tanzania na Sweden unaendana na azma ya Tanzania ya kuhamisha ushirikiano kutoka unaotegemea misaada kuelekea katika biashara na uwekezaji.
Mhe. Waziri Kombo pia ameishukuru Serikali ya Sweden kwa kuendelea kusaidia miradi ya umeme vijijini na programu za kujenga uwezo, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha mazungumzo ya kibiashara kupitia majukwaa kama makongamano ya biashara.

Kwa upande wake, Balozi Mteule wa Sweden ameeleza utayari wa nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo ya Afrika, akibainisha fursa zilizopo katika biashara, uwekezaji, nishati na maendeleo ya vijana.
Alieleza dhamira ya ya kushirikiana na Tanzania katika kuvutia wawekezaji kutoka Sweden huku akisisitiza dhamira ya Sweden ya kuendeleza uhusiano wa karibu na Tanzania uliodumu kwa miongo zaidi ya sita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here