Waziri Kombo apokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini Tanzania

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Salem Ahmed Mused Al Rashed, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Baada ya tukio hilo viongozi hao walijadili namna bora ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi.

Akizungumza na Balozi Mteule wa UAE, Mhe. Waziri Kombo amesisitiza fursa zilizopo za kuongeza biashara katika sekta za madini na usafiri wa anga, huku akibainisha umuhimu wa majukwaa ya biashara katika kuunganisha wawekezaji na wafanyabiashara baina ya nchi hizo.
Aidha, Mhe. Waziri Kombo aliishukuru kampuni ya DP World kwa mchango wake katika kuboresha ufanisi wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam na kuihimiza kuanzisha bandari kavu ndani ya nchi kwa lengo la kuongeza ufanisi wa shughuli za usafirishaji.

Pia, ameishukuru Etihad Airways kwa kuanza safari za ndege kuunganisha Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Zanzibar na kuhimiza kupanuliwa kwa safari hizo katika viwanjavya ndege vya Dar es Salaam na Kilimanjaro.
Kwa upande wake, Balozi Mteule wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ameeleza kuwa zipo fursa nyingi zenye kunufaisha Umoja wa Falme za kiarabu na Tanzania na kuahidi kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha na kuendeleza uhusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here