BoT katika Tamasha la Tatu la Fahari ya Zanzibar

ZANZIBAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inashiriki katika Tamasha la Tatu la Fahari ya Zanzibar, linalofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar kuanzia Septemba 4 hadi 14,2026.
Tamasha hilo lilifunguliwa rasmi Septemba 5, 2026 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia alipata fursa ya kutembelea banda la Benki Kuu.
Ushiriki wa Benki Kuu katika tamasha hilo unalenga kutoa elimu na uelewa kwa wananchi kuhusu majukumu ya Benki Kuu, hususan katika kusimamia na kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi, pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here