Maafisa wa Polisi waagwa kwenda mafunzoni Indonesia

DAR-Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi linaaendelea kujiimarisha katika mafunzo na kutoa huduma bora kwa wananchi limeendelea kutoa mafunzo ndani na nje ya Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo askari katika kutekeleza majukumu kwa weledi na usasa ili kufanikisha dhamira ya kutoa huduma bora kwa wananchi wanaolitegemea jeshi hilo kwa usalama wao na mali.
Akiwaaga kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Naibu Kamishna wa Polisi (DCP),Dkt. Lazaro Mambosasa amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wanaokwenda kuhudhuria mafunzo nchini Indonesia, kutumia vyema fursa hiyo kwa kuzingatia masomo watakayopatiwa na kuhakikisha maarifa na ujuzi watakaoupata unakuwa chachu ya kuleta tija, ufanisi na usasa katika utendaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, hususani katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza kuwa,Mkuu wa Jeshi la Polisi amesisitiza washiriki hao wanatakiwa kuzingatia nidhamu, weledi na maadili ya Jeshi la Polisi wakati wote watakapokuwa nchini Indonesia huku akiwataka kuwakilisha vyema Tanzania na Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha wanakuwa na mwenendo unaotoa taswira nzuri ya nchi yetu.

Aidha, amewataka washiriki hao kutumia fursa hiyo kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha sifa njema ya nchi yetu katika kudumisha amani, usalama na utulivu, pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ambapo pia amewataka kutangaza maeneo ya kipekee yenye umuhimu wa kihistoria na kiutalii, ikiwemo Bonde la Ngorongoro, ambalo ni miongoni mwa maeneo ya urithi wa dunia.
Dkt. Mambosasa amebainisha kuwa Mafunzo hayo yanatarajiwa kujikita katika maeneo mbalimbali muhimu, yakiwemo, Uongozi na Maendeleo ya Kitaaluma (Professional Development and Leadership), Ushirikishwaji wa Jamii katika Ulinzi na Usalama (Community Policing) Teknolojia Zinazochipukia (Emerging Technologies), ikiwemo Akili Bandia (AI) Matukio Makubwa na Mbinu za Uchunguzi wa Jinai (High-Profile Incidents and Criminal Investigative Techniques) Mbinu Bora za Utendaji na Ubora.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here