MANYARA-Septemba 3,2026 Mahakama ya Wilaya ya Hanang' kupitia shauri la uhujumu uchumi (ECC. No. 16332/2026) imewatia hatiani washtakiwa Bi.Anjela Matata Bio na Bw.Hussein Rajabu Mnyanke kwa kosa la wizi kinyume na kifungu cha 258(1) na 265 vya Kanuni ya Adhabu (Sura ya 16).
Kwa pamoja washtakiwa walipandishwa kizimbani kwa kosa la wizi wa Shilingi 300,000 mali ya Jumuiya ya Watumia Maji Geomi baada ya kutoa fedha hizo katika akaunti ya jumuiya kwa ajili ya kununua umeme wa kuendesha mradi na kushindwa kufanya hivyo.
Akisoma hukumu hiyo, Mheshimiwa Arnold Kileo ambaye ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang’ amewatia hatiani washtakiwa baada ya washtakiwa hao kufanya makubaliano ya kukiri kosa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Washtakiwa wameamriwa kurudisha katika akaunti ya mhanga kiasi cha Shilingi 300,000 na kulipa faini ya Shilingi 50,000. Aidha,washtakiwa wamelipa kiasi cha Shilingi 300,000 katika akaunti ya jumuiya hiyo na kulipa faini ya Shilingi 50,000 kama ilivyoamuriwa.
Shauri hilo lilikuwa limeendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Hanang’, Bw. Daudi Kingazi.
Tags
Habari
Jumuiya ya Watumia Maji Geomi
Mahakamani Leo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Tanzania
Wilaya ya Hanang
