DOHA-Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Misri, Mhe. Ahmed Kouchouk, pembezoni mwa Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar, ambapo waliangazia namna ya kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kukuza uwekezaji na kibiashara kati ya nchi hizo mbili kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.



