Mheshimiwa Deogratius Ndejembi na Guterres wazungumzia mageuzi ya UN na amani duniani

NEW YORK-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres, katika Makao Makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani, tarehe 25 Septemba 2026, ambapo amempongeza kwa uongozi wake na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake, Mhe. Guterres ameipongeza Tanzania kwa kuwa mshirika muhimu wa Umoja huo na kuthamini mchango wake katika amani na usalama duniani.
Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, yakisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kuendeleza juhudi za mageuzi, amani, usalama na ushirikiano wa kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here