Msajili wa Hazina na Barrick wajadili namna bora ya uendelezaji wa migodi

MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu leo Jumatano ya Septemba 16, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Barrick kuhusu namna bora ya uendelezaji wa migodi nchini.
Ujumbe wa Barrick uliongozwa na Afisa Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa Barrick, Bw. Woo Lee, ambaye aliambatana na Makamu wa Rais wa Masuala ya Kimataifa wa Barrick, Bw. James Ratchford, pamoja na Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Bw. Melkiory Ngido.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna bora ya kuendeleza shughuli za uchimbaji madini, pamoja na kuangalia fursa za kuimarisha ushirikiano na kuongeza manufaa yatokanayo na sekta ya madini kwa uchumi wa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here