Naibu Waziri Londo awasili Muscat kushiriki mkutano wa kwanza wa mashauriano ya kisiasa baina ya Tanzania na Oman

MUSCAT-Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb) amewasili jijini Muscat, Oman kushiriki Mkutano wa Kwanza wa Mashauriano ya Kisiasa baina ya Tanzania na Oman unaotarajiwa kufanyika Septemba 28, 2026.
Mkutano huu wa kihistoria, ambao ni wa kwanza tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Mashauriano ya Kisiasa mwaka 2009, unafanya tathmini ya jumla ya ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.


Pande zote mbili zitajadili sekta za kimkakati ikiwemo biashara, uwekezaji, madini, nishati, uchumi wa buluu, miundombinu, kilimo, elimu, utalii, urithi, utamaduni na michezo.
Mashauriano haya yanaweka msingi kuelekea Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) utakaofanyika Novemba 2026, nchini Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here