Rais Dkt.Mwinyi ashiriki sala na maziko ya Mama Fatma Karume

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameungana na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Jeneza ya Marehemu Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar.
Sala hiyo imesaliwa leo Septemba 22,2026 katika Masjid Jamiu Zinjibar, Mazizini, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini Magharibi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wanafamilia pamoja na wananchi.
Baada ya Sala ya Jeneza, Rais Dkt. Mwinyi ameungana na viongozi, wanafamilia na wananchi kuusindikiza mwili wa Marehemu Mama Fatma Karume hadi katika makaburi maalum ya familia yaliyopo Mbweni, Mkoa wa Mjini Magharibi, ambako amezikwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here