Rais Dkt.Mwinyi ateua wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano, kamati kuzinduliwa kesho Ikulu Zanzibar

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameteua wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano ambayo inawajumuisha wajumbe kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT Wazalendo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

"Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Julai 2026, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT Wazalendo vilitia saini Tamko la Pamoja la Makubaliano kuhusu Ajenda za Kufanyiwa Kazi katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu, mjini Zanzibar.

"Tukio hilo lilishuhudiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na Viongozi Wakuu wa Vyama hivyo viwili vya siasa."

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 13,2026 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,ndugu Mansura M.Kassim

"Katika kuendeleza utekelezaji wa Makubaliano hayo, hatua inayofuata ni kuundwa kwa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano. Kwa mnasaba huo, Vyama vyote viwili vimewasilisha majina ya Wajumbe waliopendekezwa kuunda Kamati hiyo."

Aidha,kwa kuzingatia mapendekezo hayo, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Abdi Mahmoud Abdi kuwa Mjumbe na Mwenyekiti Mweza wa Kamati.

Pia, amemteua ndugu Omar Ali Shehe kuwa Mjumbe na Mwenyekiti Mweza wa Kamati,Mhe. Dkt.Khalid Salum Mohamed kuwa Mjumbe, Mhe.Najma Murtaza Giga kuwa Mjumbe na Mhe.Masoud Ali Mohamed kuwa Mjumbe.

Wengine ni Mhe. Mgeni Hassan Juma kuwa Mjumbe, ndugu Omar Said Shaaban kuwa Mjumbe, ndugu Fatma Abdulhabib Fereji kuwa Mjumbe, Mhe. Said Ali Mbarouk kuwa Mjumbe na na ndugu Mohamed Nur Mohamed kuwa Mjumbe.

Vilevile,Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amewateua Makatibu Wenza na Sekretarieti ya Kamati hiyo ambapo Makatibu wa Kamati ni ndugu Mwalim Ali Mwalim na ndugu Seif Khamis Mohamed.

Kwa upande wa Sekretarieti ya Kamati walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ni ndugu Hamid Saleh Mhina, Mohamed Yusuf Nuh, Ali Salim Khamis na Abdalla Mussa Hijja.

Aidha,kamati hiyo itazinduliwa siku ya Jumatatu tarehe 14 Septemba, 2026 saa 5:00 asubuhi Ikulu, Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here