Waziri Ridhiwani Kikwete amfariji Rais Dkt.Samia

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ametoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia msiba wa mume wake,Mzee Hafidh Ameir Hassan.
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze ametoa salamu hizo za pole baada ya kushiriki na viongozi wenzake pamoja na wananchi katika kutoa heshima za mwisho na kuomboleza msiba huo uliotokea Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema, anaendelea kumuombea Rais Dkt. Samia kwa Mwenyezi Mungu ampe nguvu, subira na imani ili aweze kukabiliana na kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mwenza wake.

“Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe nguvu, subira na imani katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mwenza wake,” amesema Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete.
Pia,ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuombea marehemu na familia yake, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa pamoja na familia katika kipindi hiki cha majonzi.

Mzee Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7,2026 wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here