Wananchi walivyojumuika na maafisa usalama katika mazoezi jijini Mwanza

MWANZA-Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Matride Kuyeto leo Septemba 5,2026 akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ameongoza mazoezi ya pamoja yaliyojumuisha watumishi wa Shirika la Reli, wananchi na Askari mbalimbali kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo mkoani Mwanza kwa lengo la kuimarisha mahusiano na ushirikiano katika kulinda Miundombinu ya Shirika la Reli Tanzania.
Akizungumza mara baada ya mazoezi hayo ACP Kuyeto amesisitiza umuhimu wa mshikamano, ushirikiano na mahusiano mema baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi kwa ujumla katika kuimarisha ulinzi wa miundombinu ya Serikali ikiwemo ya Shirika Reli Tanzania akibainisha kuwa ushirikiano huo ni msingi muhimu katika kuhakikisha usalama unaendelea kuimarika.

Vilevile ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi wote ambao wapo katika maeneo yanayopitiwa na miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa kushirikiana katika kulinda vifaa vya mradi ili miradi hiyo iweze kutekelezeka kwa amani na usalama wa hali ya juu.
Aidha, aliwataka wananchi kuzingatia usalama wa reli kwa kuacha kuweka au kuondoa vitu kwenye njia ya reli.
ACP kuyeto alimalizia kwa kusisitiza kuzingatia utaratibu wa kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara,akieleza kuwa utimamu wa mwili ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uwezo wa kiutendaji na kukabiliana na maradhi mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here