BoT, Mahakama na mabenki wakutana kujadili usimamizi wa fedha za mirathi

DAR ES SALAAM- Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mahakama ya Tanzania pamoja na mabenki wamekutana na kufanya majadiliano kuhusu changamoto za Kisheria katika Mirathi, usimamizi wa mali za marehemu na uendeshaji wa akaunti maalumu ya mirathi, ijulikanayo kama Special Mirathi Account.
Special Mirathi Account ni akaunti inayofunguliwa kupitia mabenki ya biashara na msimamizi wa mirathi aliyethibitishwa na Mahakama.

Lengo la akaunti hii ni kupokea na kuhifadhi fedha za marehemu ambazo zipo kwenye benki za biashara.
Akifungua mkutano huo wa majadiliano, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kituo Jumuishi Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa, alisema umuhimu wa fedha za mirathi wa familia nyingi nchini zilipeleka kuanzishwa kwa Special Mirathi Account ambayo imesaidia kuimarisha usimamizi wa fedha za mirathi, kuongeza uwazi na kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza wakati wa usimamizi na ugawaji wa mali za marehemu.
Aliongeza kuwa utekelezaji wa akaunti hii, umeimarisha usalama wa fedha za mirathi, umeongeza uwazi na uwajibikaji, umeimarisha utekelezaji wa amri za Mahakama, umepunguza migogoro ya kifamilia na kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama na taasisi za kifedha.

Pia, alisisitiza kuwa kikao hicho kitazijadili changamoto mbalimbali zilizopo katika utejelezaji wa Special Mirathi Account ambazo ni pamoja na kutofautiana kwa taratibu na nyaraka kati ya benki moja na nyingine, uhitaji wa benki wa kuwa na njia ya haraka na ya uhakika ya kuthibitisha uhalali wa hati ya mirathi na migogoro na pingamizi kuhusu mirathi pamoja na uelewa wa wasimamizi wa mirathi na wananchi.
Kikao hicho kilifanyika Oktoba 27 2026 katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washiriki wapatao 150.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here