Jeshi la Magereza: Tundu Lissu hajagoma kula, hakuna Wakili aliyezuiwa Gerezani

DODOMA, Oktoba 27, 2026- Jeshi la Magereza Tanzania limedai kubwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu yupo salama gerezani na hajagoma kula chakula kama ilivyodaiwa, huku likikanusha madai ya kuzuiwa kwa mawakili wake watatu kuingia gerezani.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo na Msemaji wa Jeshi hilo, SACP Elizabeth G. Mbezi, Jeshi limejibu taarifa iliyotolewa Oktoba 26, 2026 na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA, Brenda Rupia, iliyodai kuwa, Lissu ameanza mgomo wa kula tangu Oktoba 26 na kuwa mawakili wake wamezuiwa.

Jeshi limesema taarifa hizo si za kweli na zinapaswa kupuuzwa, kwani ni za upotoshaji zenye lengo la kuleta taharuki kwa jamii, huku likisisitiza kuwa mawakili wanaomuwakilisha Lissu wameendelea kuruhusiwa kumuona mteja wao kwa mujibu wa taratibu baada ya kujiridhisha kuwa ni mawakili wake.

Aidha, Jeshi limewataka wananchi kupuuza na kuacha kusambaza taarifa zisizo na ukweli kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria, huku likisisitiza kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ikiwemo usalama na kuthamini utu na misingi ya haki za binadamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here