LATRA yatangaza maboresho ya barabara na njia mpya za daladala Dar es Salaam

DAR ES SALAAM-Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza maboresho ya baadhi ya barabara pamoja na njia mpya za mabasi ya mijini (daladala) jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha upatikanaji wa huduma za usafiri wa umma kwa wananchi.
Chanzo: Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LATRA Oktoba 20, 2026, maboresho hayo yanahusisha kuongezwa kwa idadi ya magari katika baadhi ya njia zilizopo pamoja na kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa huduma katika njia nyingine.

Katika maboresho hayo, njia ya Tabata Segerea–Temeke imepangiwa kuongezewa mabasi kupitia njia mbili. Njia ya kwanza inaanzia Buza Stendi, kuelekea Tabata Segerea na kupita maeneo ya Temeke Hospitali, Mandela na Bima Na. 1, huku njia ya pili ikianzia Buza Stendi, kuelekea Tabata Segerea na kupita maeneo ya Buza, Nyerere na Majumba Sita.

Kwa kila moja ya njia hizo, LATRA imeainisha mabasi 25, hivyo kufanya jumla ya mabasi yaliyopangwa kuhudumia njia hizo mbili kufikia 50.

Aidha, mamlaka hiyo imetangaza maboresho katika njia za mabasi yanayohudumia maeneo ya Mbagala na viunga vyake, hususan katika barabara ya Mbagala Kisewe–Stesheni, Mbagala Kisewe–Gerezani na Mbagala Rufu–Stesheni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabasi katika njia hizo yatapita maeneo ya Mvuti, Chamazi, Kilungule na Usalama, huku kila njia ikipangiwa mabasi 25.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha huduma za usafiri wa umma katika maeneo husika kwa kuongeza upatikanaji wa mabasi na kuboresha mtiririko wa huduma kwa abiria.

LATRA imeendelea kusimamia na kudhibiti huduma za usafiri wa ardhini nchini kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma za usafiri zilizo bora, salama na zenye ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here