Polisi watoa mbinu za kutatua migogoro ya ndoa kwa amani Kigoma

KIGOMA-Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (INSP) Spelius Rweyemamu ametoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Msambala Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma kuhusu ya mbinu bora za kutatua migogoro ya ndoa na familia kwa njia ya amani.
Akito elimu hiyo Oktoba 23, 2026 INSP Spelius amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia nguvu na vurugu pale migogoro ya kifamilia inapojitokeza. Badala yake amewasisitiza kutumia njia za kisheria na mazungumzo.

INSP Spelius amesema, migogoro mingi ya ndoa inatokana na sababu ndogo ndogo ambazo zinaweza kutatuliwa kwa urahisi kama kutokuelewana, wivu, matumizi ya pombe kupita kiasi, na ugumu wa maisha.

Kwa upande wa wananchi waliohudhuria kikao hicho wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kutoa elimu hiyo na kueleza kuwa, imewafungua macho na itawasaidia kupunguza migogoro mingi kwenye ndoa zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here