Ujenzi wa SGR Kipande cha 3 na 4, Prof. Mbarawa asema trilioni 3.67 zipo tayari

DODOMA- Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema, shilingi trilioni 3.67 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR katika kipande cha 3&4 Makutopora-Tabora na Tabora-Isaka) zipo na kwamba changamoto iliyokuwepo ni mpango kazi (workplan) wa mkandarasi, hali iliyosababisha utekelezaji wa mradi kwenda kwa kasi ya kusuasua.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo Oktoba 24, 2026 katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa reli hiyo, akibainisha kuwa hali imeanza kuimarika baada ya kazi kugawanywa katika sehemu ndogo tano ili kuongeza kasi ya utekelezaji.

Amesema, kampuni ya One Group, iliyokuwa na jukumu la ujenzi wa kilometa 100, imechukua kilometa 45, huku wakandarasi wengine wakipewa majukumu yaliyobaki

“Hakuna shida ya fedha. Shida kubwa iliyokuwepo hapa ni planning ya mkandarasi mwenyewe, kwa sababu fedhaj inaweza kuwepo lakini usipate fedha kwa sababu ya kutozalisha IPC za kutosha,” amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa amesema, shirika hilo linaendelea kusimamia wakandarasi kuhakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mipango iliyowekwa.

Amesema, mkandarasi amegawa kipande hicho katika maeneo makuu matano ya ujenzi, huku TRC ikimtaka kuwasilisha mpango kazi unaoonesha shughuli zitakazotekelezwa kila siku, ikiwemo ujenzi wa madaraja na kazi za tuta la reli.

Mhandisi Shiwa amesema kuwa, matarajio ni kuwa ifikapo mwaka 2028, mradi wa SGR katika kipande hiko utakuwa katika hatua za mwisho za ukamilishaji, hatua itakayoiwezesha nchi kusogea karibu na lengo la kutoa huduma za usafiri wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here