Rais Samia amteua Angeline Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, amtengua Beno Malisa

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Bi. Angeline Lubala Mabula.

Uteuzi huo umetangazwa leo Oktoba 28, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1. Bi. Angeline Lubala Mabula ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Bi. Mabula anachukua nafasi ya Bw. Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

2. Bw. Dunford George Mpelumbe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu ambaye amemaliza muda wake.

3. Bw. Omar Ali Omar ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Zanzibar.

Anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Khamis Hamad ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa viongozi hao wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here