SACP Sungu awapongeza askari makao makuu FFU Dodoma

DODOMA-Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Hamisi Lyanga Sungu amewapongeza askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Makao Makuu waliohudhuria mashindano mbalimbali ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania na kushinda medali pamoja tuzo.
Akitoa pongezi hizo Oktoba 23, 2026 katika Ofisi yake iliyopo Madengi Hill Ihumwa Dodoma, SACP Sungu amempongeza G.3611 SGT Rich Mathias Maduhu kwa kushiriki mafunzo ya Bomb Disposal Interaction nchini India.

Sambamba na H.4799 CPL Jofrey Juvens Mwenda kwa kushiriki mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania na Eastern Africa Police Chiefs Cooperation kuanzia mwaka 2019 hadi 2026 na kushinda jumla ya medali 12 mfululizo tangu mwaka 2019.
Vilevile, SACP Sungu amewakabidhi barua ya pongezi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura na kuwataka kuendelea kulitangaza Jeshi la Polisi kupitia michezo na kuimarisha mahusiano na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here