Ushirikiano wa kidiplomasia, Tanzania na Angola kufungua fursa mpya

LUANDA- Tanzania na Angola zimeazimia kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia kwa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kubaini fursa mpya za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Dhamira hiyo imejidhihirisha katika mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Mhe. Téte António.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili, pamoja na kubaini fursa mpya katika sekta mbalimbali zenye manufaa kwa pande zote.
Mazungumzo hayo yanaonesha dhamira ya Tanzania na Angola ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, hatua inayolenga kufungua fursa zaidi za maendeleo na kuleta manufaa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here