Dira ya 2050, Tanzania kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN)

DAR ES SALAAM- Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza dhamira ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN) katika kukuza na kulinda amani, kuimarisha taasisi za kitaifa na kuendeleza maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Ulega (Mb), amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 81 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Oktoba 23, 2026.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano huo kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa ili kuhakikisha unaleta matokeo yenye manufaa kwa wananchi wetu, na Tanzania inathamini uhusiano wake na Umoja wa Mataifa, Uhusiano huu umetoa mchango muhimu katika kuimarisha taasisi za kitaifa, kusaidia programu za maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini na kukuza ushirikiano wa kimataifa kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa,” alisisitiza.
Akizungumzia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mhe.Waziri Ulega amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, Umoja wa Mataifa na wadau wa maendeleo katika kuwekeza kwa wananchi, kuimarisha taasisi, kukuza ubunifu na kupanua fursa za kiuchumi na kubainisha kuwa uwezeshaji wa wanawake na vijana kupitia elimu, mafunzo ya ujuzi, ujasiriamali, upatikanaji wa mitaji na fursa za ajira ni muhimu katika kufanikisha maendeleo jumuishi na endelevu.

Kuhusu umuhimu wa kudumisha amani, umoja wa kitaifa, maridhiano na utawala jumuishi, alieleza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kujenga taifa lenye ustawi na ustahimilivu na kuongeza kuwa Tanzania inaendelea kuunga mkono ushirikiano wa kimataifa, utatuzi wa migogoro kwa njia za amani.
Maadhimisho ya 2026 yameendeshwa chini ya kaulimbiu isemayo “Miaka 81 ya Umoja wa Mataifa: Kujenga Mustakabali wa Amani, Utu na Uendelevu kwa Wote.” (81 Years of United Nations: Building a Future of Peace, Dignity, and Sustainability for All) ambayo inasisitiza wajibu wa pamoja wa mataifa katika kujenga dunia yenye amani, maendeleo jumuishi na endelevu yenye manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Siku ya Umoja wa Mataifa duniani hutoa fursa ya kutafakari mafanikio ya Umoja ya Mataifa tangu ulipoanzishwa 1945, kuthibitisha misingi na madhumuni ya Mkataba wa kuanzishwa kwa umoja huo na kuhuisha dhamira ya pamoja ya kushirikiana katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Wanadiplomasia, wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, washirika wa maendeleo, Asasi za kiraia, viongozi wa dini, sekta binafsi, makundi ya vijana na wanawake.

Maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa hutoa fursa ya kutafakari mafanikio ya Umoja ya Mataifa tangu kuanzishwa kwake 1945, kuthibitisha tena misingi na madhumuni ya Mkataba wa kuanzishwa kwa umoja huo, pamoja na kuhuisha dhamira ya pamoja ya kushirikiana katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here