Yanga yavunja mkataba na Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Young Africans Sports Club umesema kuwa, umefikia uamuzi wa kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu ya kwanza, Manqoba Mngqithi.
Manqoba Mngqithi.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 24, 2026 na Afisa Mtendaji Mkuu wa Young Africans Sports Club, Andre Mtine.

Vile vile, Uongozi wa Young Africans Sports Club umesitisha mkataba na Kocha wa Viungo wa timu ya kwanza, Chyna Mokaila.

"Uongozi unawashukuru Watendaji hawa kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri kwenye majukumu yao mapya.

"Tayari mchakato wa haraka wa kumpata Kocha Mkuu mpya umeanza na unatarajia kukamilika hivi karibuni."
Aidha, uamuzi huo unakuja saa chache baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kulazimishwa sare na TRA United katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga SC kubaki na pointi 19 baada ya kucheza michezo nane, huku watano wao wa jadi, Simba SC, wakiendelea kuongoza msimamo wa ligi kwa pointi 24 baada ya kucheza michezo nane.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here