Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo Desemba 3,2021

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.
Rais Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi ameteua wafuatavyo;

Mosi, Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Mohammed Amour Mohammed kuwa, Mhasibu Mkuu wa Serikali.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Fatma Khamis Mohamed kuwa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.

Aidha,kwa mujibu wa taarifa ya Mhandisi Zena A.Said uteuzi huo umefanyika leo Desemba 3,2021 na unaanza leo Desemba 3,2021.

Post a Comment

0 Comments