Wachezaji KMC FC wajinoa kuikabili Azam FC

Nahodha wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC,Juma Kaseja pamoja na David Brayson wameungana na wachezaji wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ikiwa ni baada ya kutoka katika kikosi cha Timu ya Taifa Taifa Stars katika mchezo wa kufuzu kombe la Afrika (AFCON 2021).

Mbali na Kaseja, Brayson ,wengine waliorejea kuungana na kikosi cha KMC FC ni Kocha wa Magolikipa wa timu hiyo, Fatuma Omary ambaye aliitwa kufundisha magolikipa wa Timu ya Taifa ya Wanawake U-17 katika michuano ya kuwania ubingwa wa kombe la COSAFA.
Kocha msaidizi wa Timu ya KMC FC, Habibu Kondo mwenye kofia, akiwa na Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Simkoko akitoa maelezo kwa wachezaji hawapo pichani wakati walipokuwa wakifanya mazoezi.
Nahodha wa Timu ya KMC FC, Juma Kasema akiwa kwenye mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam.
Wachezaji wa Timu ya KMC FC wakiwa mazoezini.

Aidha, KMC FC hivi sasa inaendelea kufanya maandalizi katika kuelekea mchezo wa mzunguko wa 12 wa ligi kuu ambapo itakutana na Azam Jumamosi ya Novemba 21 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni wenyeji wa mchezo huo.

Hata hivyo katika kikosi hicho, wachezaji wawili bado hawajarejea kambini ambao ni pic Ally ambaye alifiwa na Baba yake mzazi pamoja na Rahim Sheihe ambaye bado yupo katika Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes.

Kwa mujibu wa Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya KMC FC,Christina Mwagala hadi sasa kikosi cha KMC FC hakina majeruhi na kwamba mchezaji ambaye alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Gwambina Misungwi mkoani Mwanza, Emmanuel Mvuyekule amesharejea mazoezini na anaendelea vizuri.

Post a Comment

0 Comments