Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wameieleza Diramakini kuwa, ajali hiyo imetokea wakati gari moshi hilo likitokea jijini Dar es Salaam kuanguka na kusababisha vifo kadhaa, majeruhi na yenyewe kuharibika vibaya.

Afisa mmoja kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa sharti la kuoandikwa jina lake amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo ingawa hakuwa tayari kutoa maelezo kwa kina. "Ndiyo imetokea, ila ni suala la muda, mamlaka husika watatoa taarifa muda ukifika,"amedokeza Afisa huyo. Endelea kufuatilia hapa kwa kina zaidi...
Mashuhuda wameieleza Diramakini kuwa, juhudi za Serikali zinaendelea kuhakikisha huduma za uokozi zinatolewa mapema na tayari Mkuu wa Wilaya ya Bahi amewasili katika tukio hilo.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amethibitisha kwamba, treni hiyo ya abiria iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Bara imepata ajali wilayani Bahi umbali wa kilomita 40 kutoka jijini Dodoma,
"Tunaandaa mabasi ya kwenda kuchukua abiria pale wawapeleke Manyoni, kuna treni yetu ya abiria inatoka Bara, wanaoendelea na usafiri Bara waingie huko waendelee na safari, na waliokuwa wanatoka Bara kuelekea Dar es Salaam waingie kwenye mabasi wawalete Dar es Salaam,"amesema.


Wakati tunaendelea kusubiri Taarifa Sahihi na takwimu za ajali, tutambue Hiyo Ni Ajali kama ajali nyingine, tujipe muda
ReplyDeletePoleni sana wahanga wa hii ajali
ReplyDeleteThanks for news
ReplyDelete