Ajali ya treni yaua, yajeruhi Kanda ya Kati jijini Dodoma


Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya ajali ya treni iliyotokea leo Janurai 2, 2021 kati ya Stesheni ya Bahi na Itigi maeneo ya Kanda ya Kati jijini Dodoma, anaripoti Mwandishi Diramakini. 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wameieleza Diramakini kuwa, ajali hiyo imetokea wakati gari moshi hilo likitokea jijini Dar es Salaam kuanguka na kusababisha vifo kadhaa, majeruhi na yenyewe kuharibika vibaya.

Afisa mmoja kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa sharti la kuoandikwa jina lake amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo ingawa hakuwa tayari kutoa maelezo kwa kina. "Ndiyo imetokea, ila ni suala la muda, mamlaka husika watatoa taarifa muda ukifika,"amedokeza Afisa huyo. Endelea kufuatilia hapa kwa kina zaidi...

Mashuhuda wameieleza Diramakini kuwa, juhudi za Serikali zinaendelea kuhakikisha huduma za uokozi zinatolewa mapema na tayari Mkuu wa Wilaya ya Bahi amewasili katika tukio hilo.
 
TRC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amethibitisha kwamba, treni hiyo ya abiria iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Bara imepata ajali  wilayani Bahi umbali wa kilomita 40 kutoka jijini Dodoma,

"Treni ilikuwa na watu zaidi ya 700,  kuna mvua zinanyesha sana, bado hatujajua chanzo cha ajali ila kichwa kimeanguka, taarifa za awali zinaonesha mfanyakazi wetu mmoja amefariki na abiria wawili wamefariki, nilikuwa likizo nimeikatisha naelekea eneo la tukio sasa.

"Tunaandaa mabasi ya kwenda kuchukua abiria pale wawapeleke Manyoni, kuna treni yetu ya abiria inatoka Bara, wanaoendelea na usafiri Bara waingie huko waendelee na safari, na waliokuwa wanatoka Bara kuelekea Dar es Salaam waingie kwenye mabasi wawalete Dar es Salaam,"amesema.

Mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu kutoka Sekta ya Afya jijini Dodoma ametoa wito kwa wauguzi na madaktari popote walipo usiku huu kwenda Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma ili kuunganisha nguvu ya kutoa huduma kwa wananchi ambao wamepata ajali.
 
"Ndugu yangu hili ni tukio la ghafla sana, na watu ni wengi ambao walikuwa katika treni, hivyo ni wito wangu kwa wataalamu hao wa afya popote walipo na wanaosoma Diramakini waweze kuja usiku huu tuweze kuwasaidia Watanzania wenzetu,"ameeleza.

Post a Comment

3 Comments

  1. Wakati tunaendelea kusubiri Taarifa Sahihi na takwimu za ajali, tutambue Hiyo Ni Ajali kama ajali nyingine, tujipe muda

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wahanga wa hii ajali

    ReplyDelete